Yeah! Ukiwa na wakati fanya la wakati/Nina matatizo makubwa matatu(3) moja kubwa ni pesa lapili ni mapenzi na la mwisho kabisa ni umaarufu/Nikiambiwa ni chague moja fasta fasta nitachagua pesa maana ndio naona ina kila kitu/Japo Mwenyez Mungu wangu ndo kila kitu/Hakuna naye mwamini chini ya jua zaidi ya mungu wangu/Sitajichanganya hata kwa dawa kumwamini mpenzi wangu/Nguzo yangu kuu ni muumba wangu/Mfariji wangu nikiwa sina kitu mfukoni mwangu/Mawazo na matumaini na hata malengo yangu yeye ndio anaye weza kuyatimiza na kuniliwaza kwa kilakitu maishani mwangu/Baba kajaza chuki dhidi yangu/Upole wa Mama yangu ndio dhiki yangu/Upofu wangu ndio furaha ya Baba yangu/Fikra zangu zinawafurahisha wengi hata uwezo wangu wakuwashauri unawavutia ndugu zangu/Ipo siku nami nitayafurahia mawazo yangu/Siku maombiyangu yatakapo jibiwa na mwenyezi Mungu wangu.















